Jumamosi 14 Machi 2026 - 06:00
Shirika la Waislamu wa Kishia la Urusi lampongeza Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei

Hawza/ Jaffarov, Rais wa Shirika la Waislamu wa Kishia Urusi, katika ujumbe wake ametoa pongezi kwa kuchaguliwa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei kuwa kiongozi wa tatu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Jaffarov, rais wa Shirika la Waislamu wa Kishia la Urusi, katika ujumbe wake ametoa pongezi kwa kuchaguliwa kwa Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei kuwa kiongozi wa tatu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Dkt. Kazem Jalali
Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Urusi

Kwa heshima kubwa,

Kwa mara nyingine tena napenda kutoa pole zangu za dhati kutokana na shahada ya kiongozi wa kiroho wa Iran, Sayyid Ali Khamenei (r.a), na wakati huo huo ninatoa pongezi kwa taifa la Iran kwa kuchaguliwa kwa Mtukufu Mojtaba Hosseini Khamenei kuwa kiongozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Nina yakini kwamba shughuli na juhudi zake katika jukumu hili tukufu zitachangia zaidi maendeleo ya Iran na kulinda pamoja na kuhifadhi maslahi ya kitaifa ya nchi hiyo. Katika kipindi hiki kigumu, ninawatakia taifa la Iran pamoja na kiongozi wake mpya subira, uthabiti na mafanikio katika kushinda changamoto zote.

Ninatumaini kwamba; mazungumzo yenye kujenga na kuimarishwa kwa uhusiano wa pande mbili kwa njia ya kina vitaendelea; jambo ambalo nafasi yako kama mkuu wa ujumbe wa kidiplomasia ina thamani kubwa na mchango wake ni wa msingi.

Kutoka moyoni ninakutakia afya njema, mafanikio na ushindi mpya katika kutekeleza majukumu yako mazito.

Kwa heshima,

Kwa niaba ya Shirika la Waislamu wa Kishia,
Familia Jaffarov.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha